Posted by Williammalecela.com on Tuesday, April 21, 2015
Mwili
wa Muhadia Juma ukizikwa. Muhadia alichukuliwa kijijini kwao na
kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mafia kwa matibabu na mkuu wa wilaya
hiyo, Dk. Nassoro Hamid aliyepata taarifa za kufungiwa ndani kwa miaka
kumi na mama yao kupitia gazeti hili toleo la Machi 31, mwaka huu
lililokuwa na kichwa cha habari ‘MAMA AWAFUNGIA NDANI WANAYE 3 KWA MIAKA
10.’
BINTI Muhadia Juma ambaye alikuwa mmoja wa watoto
watatu waliofungiwa ndani ya nyumba kwa miaka kumi na mama yao mzazi,
Mwasiti Ally katika Kijiji cha Kanga, wilayani Mafia amefariki dunia
Aprili 15, mwaka huu.Huyu ni kijana wa pili kufariki dunia baada ya
Ally Juma kuaga dunia hivi karibuni na kufanya aliyebaki hai kuwa mmoja,
Mzee Juma.
Habari kutoka Mafia zinasema Muhadia baada ya
kufikishwa hospitalini, alianza kupatiwa matibabu na lishe bora lakini
siku hiyo ya kifo chake (Aprili 15) hali yake ilibadilika ghafla na
kuaga dunia saa 1.30 usiku.Marehemu huyo alizikwa Aprili 16, mwaka huu
katika Kijiji cha Kanga kilichopo kilomita 40 kutoka Mafia mjini ambapo
gharama zote za mazishi ziligharamiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya.
Muhadia
Juma enzi za uhai wake. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu
juzi, Mkuu wa Wilaya, Dk.Hamid alisema amesikitishwa na vifo vya ndugu
hao wawili waliokufa kwa mateso makubwa na ya muda mrefu.“Ni bahati
mbaya sana ofisi yangu ilipata taarifa juu ya wagonjwa hao wakiwa katika
hali mbaya. Nitoe wito kwa wananchi kwamba wanapokuwa na matatizo kama
hayo wasifiche, watoe taarifa serikalini ili washughulikiwe mapema,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment