kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni migogoro ya mara kwa mara.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi wetu waliwaendea hewani kwa nyakati tofauti, Mike na Thea ambapo kila mmoja alifunguka kivyake. “Mh nani kawaambia maneno hayo? Watu wanapenda kuzusha sana, mimi najua mke wangu bado nipo naye amekwenda kwao kupumzika atarudi,” alisema Mike.
Kwa upande wake Thea alifunguka: “Mmh, hakuna kitu kama hicho nani aliyewaambia, Mike kama amesema nimeenda kupumzika anajua yeye, kwanza naenda kupumzika nina mimba? Mimi nilikuwa ‘production’ na hivi ndiyo narudi nyumbani nikifika nitakupa simu uongee na Mike.”Hadi gazeti hili linakwenda mtamboni Thea hakuwasiliana na mwandishi ambaye anasubiri simu yake mpaka sasa
0 comments:
Post a Comment