Gladness Mallya
MSANII mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ ameibuliwa kutoka mafichoni na kueleza kuwa, hajafulia kama baadhi ya watu wanavyofikiria.
Akistorisha na gazeti hili hivi karibuni, Nora ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu alisema anawashangaa watu wanaozusha kwamba amefulia wakati maisha yake anayaendesha kama kawaida. “Mimi sijafulia jamani, nipo na nitazidi kuwepo na mashabiki wangu wajue kwamba kimya kingi kina mshindo mkuu, kisanii nipo chimbo naandaa mambo mazuri,” alisema Nora.
0 comments:
Post a Comment