Shahidi
wa nne katika kesi ya tuhuma za ubakaji inayomkabili Emmanuel Mbasha,
mume wa mwanamuziki wa nyimbo za injili, Flora Mbasha, jana alidai
mahakamani kuwa hakuona dalili zozote za kuingiliwa kimwili mlalamikaji.
Hayo yalidaiwa na daktari wa Hospitali ya Amana, Migole Mtuka, ambaye alimfanyia vipimo msichana huyo.
Daktari
huyo alidai katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwamba vipimo
alivyomfanyia msichana huyo anayedaiwa kubakwa na Mbasha, havikuonyesha
kitu chochote.
Dk. Migole alidai kuwa binti huyo alifika hospitalini hapo Mei 26, mwaka jana, kwa alili ya kufanyiwa vipimo.
Alidai
kwamba binti huyo alipofika hospitalini hapo, alimfanyia kwanza vipimo
vya macho kisha kumtaka kwenda kufanya vipimo vya maabara, ambavyo
hutolewa bure.
Dk.
Migole alidai kwamba baada ya kumtaka kwenda kufanya vipimo vya
maabara, akiwa na baadhi ya ndugu wa familia yake, hakwenda bali
aliingia mitini na kurejea Juni 3, mwaka jana, baada siku nane kupita.
Alidai
baada ya kufanyiwa hivyo, vipimo hivyo vilionyesha kuwa hakuna kitu
chochote alichofanyiwa, kwa maana ya kubakwa au kuingiliwa na mwanamume
katika mwili wake na kuwajazia fomu aina ya PF3 kwa kile alichokiona.
“Binti
huyo hakuonekana kuwa na ujauzito, maambukizi ya virusi vya ukimwi
(VVU) na wala mbegu za kiume katika sehemu za siri,” alidai daktari
huyo.
Hata
hivyo, baada ya kutolewa ushahidi huo, Hakimu Flora Mujaya, hawakuweza
kusikiliza ushahidi mwingine kutokana na taarifa za msiba wa hakimu
mwenzao, zilizofika mahakamani hapo.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa upande wa Jamhuri Aprili 20, mwaka huu.
Mbasha
anadaiwa kuwa Mei 23 na 25, mwaka jana, alimbaka binti mwenye umri wa
miaka 17, ambaye anadaiwa ni shemeji yake huku akijua kufanya hivyo ni
kinyume cha sheria.

0 comments:
Post a Comment