KUFUATIA
kauli ya Wema Sepetu ya hivi karibuni kuwa hawezi kupata mtoto wa
kumzaa, mastaa wa fani mbalimbali wamejitokeza kumtuliza moyo,
wakiongozwa na hasimu wake wa karibu, Kajala Masanja, ambaye amesema
hana sababu ya kukata tamaa, kwani bado ni mdogo.
Akizungumza
na gazeti hili baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea masikitiko
yake juu ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema anaamini hana
tatizo kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa anadhani bado
hayampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza kumsaidia
tatizo alilonalo.
“Namuombea
sana kwa Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi kupata mtoto
katika maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu bwana,” alisema
Kajala, ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini, roho inaniuma
sana, namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge.
Na watu
waache kumuumiza kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari
kulea mtoto wa mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na
kumtunza kama wake.
Wastara Juma.
“Naomba
achukue mfano wangu mimi Wastara, Mungu kanipokonya mguu kanipa watoto,
natumia mguu wa bandia na ninatembea lakini Wema amepewa kila kitu
kasoro mtoto, atumie mtoto ambaye siyo wa kumzaa amlee kama wa kwake na
hapo machungu, huzuni na mawazo vitaisha na atamzoa kama wa kwake,”
alisema Wastara Juma.
Wengine
waliompa pole na kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni pamoja na
Jini Kabula, Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na Baby Madaha
ambaye alisema;
Aisha Bui.
“Mtoto siyo
mwisho wa maisha, kuna mastaa wengi tu ambao hawana watoto na wanaishi
kwa amani kama Oprah, Tyra Banks na wengineo, hivyo siyo ishu kubwa
kihivyo, watu waache kumsakama Wema, mimi mwenyewe sina mpango wa kuwa
na mtoto.”
0 comments:
Post a Comment