1.Siwezi kuwa ulivyo,
Maana hatufanani.
Siwezi kuwa mlivyo,
Maana hatulingani.
2.Siwezi kukuchukia,
Napata faida gani?
Huenda nikanyamaza,
Niseme faida gani?
3.Na siwezi kukimbia,
Nitafika polepole.
Naepuka kujikwaa,
Ili nisiangamie.
4.Na siwezi kukuacha,
Amini ahadi yangu.
Mimi na wewe daima,
Amini maneno yangu.
5.Siwezi u malaika,
Na mimi ni binadamu.
Siwezi ya kujifanya,
Ninayo makosa yangu.
6.Na siwezi kunyamaza,
Kuacha wewe ulie.
Siwezi kujikunyata,
Kuacha wewe upigwe.
7.Siwezi ya unafiki,
Eti kujikombakomba.
Kujifanya ni rafiki,
Daima kuombaomba.
8.Siwezi tupa imani,
Muumba wangu daima.
Siwezi acha imani,
Dunia kutangatanga.
9.Siwezi kuwa sungura,
Wakati mimi ni tembo.
Daima mimi ni simba,
Naishi kama nilivyo.
10.Na siwezi kukudhuru,
Faraghani hadharani.
Siwezi kukupa sumu,
Ya unga au majani.
11.Nasema leo ujue,
Tuishi kama jamaa.
Nasema leo mjue,
Tuishi kifamilia.
12.Ni kwa tungo na vijembe,
Kutunga kutungiana.
Kwa visu pia viwembe,
Kama maji, kama jua.
Tenzi za Almasi.
MDUARA WA DUARA.
tanganyumbani@gmail.com |
Wednesday, April 22, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment