“Huyu mchungaji wa siku zote ni mtu mstaarabu sana, hana maneno na mtu, lakini huyu mwanamama ni mtata kwelikweli,” kilisema chanzo hicho.KATIKA tukio lililowaacha watu midomo wazi wasiamini kilichokuwa kikitokea, waumini wa Kanisa la Moravian Usharika wa Boko nje kidogo ya Jiji la Dar, walishuhudia timbwili la aina yake, baada ya waumini kugawanyika pande mbili na kuanza kuvurumishiana makonde wakigombea madaraka.
Kuonyesha kuwa shetani amekuwa na nguvu kubwa katika jumuia hiyo ya kiroho, makundi ya wafuasi hao wamekuwa wakifanyiana visa, kiasi kwamba kundi mojawapo linapowahi na kufanya ibada, hufunga mlango kwa kufuli aina ya solex ili kuwazuia wenzao kufanya maombi na hivyo kuzidisha uhasama kati yao.
Hata hivyo, katika hali isiyotarajiwa, baadhi ya waumini waliotengana waliamua kumaliza tofauti zao na hivyo kuanza kusali pamoja, hali ambayo badala ya kuleta amani sehemu hiyo takatifu, ilizidisha tafrani na kusababisha kuzuka kwa ugomvi uliosababisha baadhi ya viongozi wa kanisa hilo kuchaniwa mashati.
Baada ya mvutano wa muda mrefu wa kupigana, kutukanana, kuchafuana na kuchaniana nguo, hatimaye Polisi wa Kituo cha Wazo Hill, walifika eneo la tukio na kumaliza ‘soo’ hilo kwa kuwakamata na kuondoka na watuhumiwa pamoja na baadhi ya waumini.
Hata hivyo, Mchungaji Samweli ambaye naye alikamatwa, aliachiwa baada ya kumaliza kutoa maelezo yake.
0 comments:
Post a Comment