Tetekuwanga kitaalamu Chicken Pox, ni ugonjwa unaombukiza na kusababishwa na virusi vinavyojulikana kama Varicella zoster virus.Maambukizi ya tetekuwanga huonekana sana kwa watoto wadogo ingawa hata watu wakubwa pia huyapata.
Katika nchi zenye kupata majira ya baridi, maambukizi ya ugonjwa huu huonekana sana wakati wa kipindi cha majira ya baridi na kipindi cha masika.
Maambukizi ya tetekuwanga wakati wa ujauzito yanaweza kuathiri mtoto hasa kama mama atapata maambukizi haya wiki 28 baada ya kushika mimba.Wanawake ambao wana kinga dhidhi ya ugonjwa huu hawawezi kupata tetekuwanga kipindi cha ujauzito na wasiwe na wasiwasi kuhusu mtoto wao kupata madhara.
Madhara ya tetekuwanga kwa mtoto ni kutokana na uwezo wa Varicella zoster virus kuwa na uwezo wa kuvuka kondo la uzazi (placenta) kutoka kwa mama mwenye tetekuwanga na hivyo kumuathiri mtoto.
Maambukizi ya tetekuwanga kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kipindi cha ujauzito hujulikana kama Fetal varicella syndrome au congenital varicella syndrome na huambatana na madhara kwenye ubongo wa mtoto-(Kichwamaji yaani hydrocephalus), kichwa kuwa kidogo, maambukizi ya ubongo (encephalitis), aplasia of brain.Madhara ya macho kama mtoto wa jicho (cataract), madhara ya mishipa ya fahamu, madhara ya kibofu cha mkojo, miguu, njia ya haja kubwa,vidole kutoota vizuri n.k.
0 comments:
Post a Comment