Gari lililopata ajali
Zaidi ya watu 22 wamepoteza maisha huku 30 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria kuingia mtaroni katika mji wa Kashmir nchini India leo jumatatu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu kamishna wa wilaya ambapo gari hilo limeanguka alisema kuwa waliweza kuitambua miili 22 hadi sasa na bado upo uwezekano wa kuwepo kwa miili mingine iliyonasa chini ya gari .
Afisa mmoja amesema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba zaidi ya watu 60 katika safari yake.
Afisa huyo aliongeza kuwa “Basi hilo liliacha barabara na kubiringita chini kwenye mtaro wa Maroti wilaya ya Udhampur.
Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
0 comments:
Post a Comment