LEMUTUZ

Tuesday, May 12, 2015

BAHATI BUKUKU ANASUMBULIWA NA NJAA AU NI MAPENZI YAKE KWA MGOMBEA URAIS WA CCM? SOMA HABARI KAMILI HAPA LIVE!!

Posted by Williammalecela.com on Tuesday, May 12, 2015
Malisa Godlisten
MUOGOPENI BAHATI BUKUKU.!

Nimesikitika sana kuusikia wimbo wa Bahati Bukuku aliomuimbia Lowassa na kumpamba kuhusu mbio zake za Urais. Sina tatizo la Lowassa kutafuta Urais maana ni haki yake kikatiba. Ana haki ya kugombea, kupigiwa kura na hata kushinda. Ila nina tatizo na Bukuku aliyeamua kuacha kumuimbia Mungu na kumtukuza mwanadamu.


Nimeainisha makosa 10 ya Bahati Bukuku yanayohusiana na wimbo huo;

1. Bukuku anasema Lowassa atatawala kwa amani na ubora ambao Rais yoyote hataweza kufikia. Hapa kuna makosa mawili. La kwanza ni kusema atatawala.

Nani kamhakikishia Bukuku kuwa Lowassa atatawala? Hivi Bukuku anajua kuwa jina la Lowassa linaweza kupelekwa NEC na lisirudi? Au likarudi halafu wananchi wakamkataa? Sasa yeye anajihakikishiaje kuwa Lowassa atatawala?

2. Pili kasema Lowassa ataongoza kwa ufanisi kuliko wote waliomtangulia na watakaomfuatia. Huu ni ujuha wa kiwango cha "PhD". Hivi unawezaje kupima uwezo wa mtu kabla hajafanya kazi? Ni sawa na kununua nguo za mtoto wa kiume kisa mkeo akiwa na mimba alipenda kula sana ugali, mwishowe anazaliwa wa kike..!

3. Bukuku anasema Lowassa ana hekima kama Suleimani. Hii ni kufuru kubwa kwa Mungu. Maandiko yanasema hakuwahi kutokea mtu mwenye hekima kama Suleimani na hatatokea. Sasa Bukuku kamtoa wapi Lowassa? Ina maana Bukuku ana akili kuliko Mungu aliyeruhusu maandiko hayo?

4. Bukuku anasema Lowassa amepakwa mafuta kama Daudi. Maandiko yanasema Daudi alikuwa Mteule wa Mungu na alipakwa mafuta na Kuhani mkuu Samuel. Kujaribu kumfananisha Lowassa na Daudi ni makosa makubwa. Ni Kuhani gani amempaka mafuta Lowassa? Labda Kuhani Yusuph Makamba.. Na alimpaka mafuta gani? Ya Alizeti au Baby Care.!

5. Si sahihi kwa mtumishi wa kiroho kumfanyia kampeni mgombea waziwazi. Either ni Mchungaji, Padri, Askofu, Sheikh, Ustaadh etc sio sahihi kumsifia mgombea hadharani. Kama unampenda mgombe ibaki moyoni mwako na ufanye maamuzi mwenyewe bila kushawishi wengine.

6. Kumpigia debe mgombea ni kuwagawa waumini. Kuna wafuasi wa Bahati Bukuku hawamkubali Lowassa, sasa haoni anawakwaza?

7. Pia Kuna wafuasi wa Lowassa si Wakristo. Wengine ni waislamu na wengine hawana dini. Sasa Bukuku haoni anawakwaza kwa wimbo wake?

8. Wimbo huu unaibua chuki za kidini na kuonekana Lowassa yupo kwa ajili ya wakristo tu. Kama Lowassa anawapenda pia Waislamu mbona hatujasikia akiimbiwa "Kaswida"? Kumuimbia "mapambio" tu ni ishara ya kuwatenga waislamu na kuwaonesha kuwa Lowassa si mtu wao.

9. Wimbo huu unajenga ushawishi upande mmoja tu wa wakristo. Mbona Waislamu hawakuguswa na wimbo huu? Hivi unawezaje kumshawishi Muumini safi wa kiislamu amkubali Lowassa kwa kusikiliza Pambio??

10. Wimbo huu umemfanya Bukuku kuonekana "Changudoa wa kiroho". Hawezi kuwacheka wanawake wanaouza miili yao kwa fedha, maana na yeye kauza utu wake wa kiroho kwa tamaa ya fedha na mali za dunia.

NB: Kwa ujumla Bukuku amejipunguzia sana heshima yake mbele ya jamii. Waislamu wamemuona ni mdini, wakristo tumemuona mnafiki. Wapo wakristo kadhaa waliojiapiza kutonunua tena kazi zake kutokana na upuuzi alioufanya.

Najua njaa ya pesa ndiyo imemfanya akaamua kuwa vuvuzela la Lowassa. Lakini kwa heshima kubwa aliyokua ameijenga kwenye jamii ni bora asingefanya hiyo kazi. Bora angekubali kukosa hizo hela kuliko upuuzi alioufanya. Njaa ya siku moja haiuwi.
Pesa alizozipata atazitumia na zitaisha lakini doa alilojiwekea halitatoka hata siku anaingia kaburini.

Muasisi wa taaluma ya Public Relations, Arthur Page aliwahi kusema "You may need 20 years to build your reputation, but it takes only 5 seconds to destroy it". Akimaanisha unaweza kutumia miaka 20 kujenga haiba yako mbele ya jamii lakini sekunde 5 tu zinatosha kuharibu kile ulichokijenga kwa miaka 20. Na hivi ndivyo alivyofanya Bahati Bukuku. R.I.P Bukuku.!
Malisa Godlisten's photo.

  • Mushi Michael, Goodluckies Good, Rukia Gamba and 110 others like this.
  • Babuu Makundi Walaaniwe wamtegemeao mwanadumu na kuabudu miungu mingine isipokuwa Mungu
    Like · Reply · 9 hrs
  • Nkoswe Mwanalyela Ole Wenu Mzifanyazo Nyumba Za Ibada Kuwa Vichaka Vya Kuficha Maovu Yenu,usifanye Kapeni Za Siasa Ktk Nyumba Ya Ibada.
    Like · Reply · 9 hrs
  • Erick Mtani Tanzania ya Leo pesa inanunua utu wa mtu,pesa inanunua mpaka Maaskofu,Majaji,usishangae hapo hapo hakuna kitu wasanii wetu wa dini wanaimba lkn hawaishi kweny yale wanayoimba...
    Like · Reply · 1 · 8 hrs
  • Josephat Mwambola ALIYEAMINIKA KUWA NI MTUMISHI WA MUNGU,KAFANYA BIASHARA HARAMU...ANZA KUIMBA TAARABU BAHATI BUKUKU,INJIRI UMEINAJISI
    Like · Reply · 8 hrs
  • Khadija Lujula huyu n mfanyabiashara
    Like · Reply · 1 · 8 hrs
  • Haji Kipanga Huo wimbo ni bora mara elfu 10 kusikiliza hata nyimbo za bongo fleva kuliko huo upuuzi, tena huyo angekua ni muislam alitakiwa acharazwe bakora kwa kuharibu maandiko ana bahati sana wakristo ni wapole ila kawadhalilisha walokole kwa huo upuuz, nashauri apuuzwe tu yy na huyo anaemkampenia
    Like · Reply · 8 hrs
  • Andrew Samson kichwa maji huyo hawezi kupewa rushwa na kupelekwa studio aibu tupu
    Like · Reply · 8 hrs
  • Mpoki John Poor Bahati, what a shame?
    Like · Reply · 7 hrs
  • Ntuly Dunga Duh
    Like · Reply · 7 hrs
  • Goodhelp Mwanginde Bahati bukuku unaharibu neno LA mungu kwa tamaa ya pesa
    Like · Reply · 7 hrs
  • Goodhelp Mwanginde Bora nisikilize nyimbo za dansi kuliko kusikiliza nyimbo bahati bukuku
    Like · Reply · 7 hrs
  • Daudi Nyagawa Duu dada heshima yake yapoteya kwasababu yapesa
    Like · Reply · 7 hrs
  • Profesa MichaelSele Wa San-siro Bahati Bukuku ni mfuasi wa shetani
    Like · Reply · 7 hrs
  • Johnie M Bentraud Ndo wachumia matumbo wa sikuhizi hao, keshapeww chake ndo anapamba watu kwa mapambio, Mungu hapendi hayo dada bukuku.
    Like · Reply · 7 hrs
  • Mabula Felix Wacha mungu wanafanya dhambi mpaka shetani anaogopa!!
    Like · Reply · 7 hrs
  • Happy Katabazi Mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo,ulidhika kuwa nacho japo hakina thamani.
    Like · Reply · 7 hrs · Edited
  • Eliaringa Macha Waimbaji wa nyimbo za injili kwa sasa ni wakuogopa sana hata maandiko yameandika na alaaniwe yule amtegemea mwanadamu sasa huyu bukuku haoni kama hii ni kufuru kwa mola aliye muumba
    Like · Reply · 6 hrs
  • Eliaringa Macha Anahubiri Injili gani sasa? HUU NI ULIMBUKENI HASWAA WA KUPENDA PESA KULIKO ROHO ZA WENZAKO. R. I. P
    Like · Reply · 6 hrs
  • Jaqckline S Jordan duu..
    Like · Reply · 5 hrs
  • Bornface Njechele Wanasiasa wengi, hasa walio waroho wa madaraka na waliolewa UTAMU wa "Keki ya Taifa", aina ya kina #Lowassa, huwa wanautumia "Upeo Mdogo Wa Watanzania na "Tamaa Ya Pesa" kuwa mitaji yao katika kuhakikisha wanaendelea kuitafuna nchi, na pengine hadi ku...See More
    Like · Reply · 1 · 5 hrs
  • Beatrice Vedastuce Mh!
    Like · Reply · 5 hrs
  • Kagisa Simon
    Like · Reply · 3 hrs
  • Young Fledy Kweli dunian kunawatu ..naviatu
    Like · Reply · 3 hrs
  • Theobard Zeno Njia moja na mwenzie flora mbasha acha waabike ili wajifunze.
    Like · Reply · 3 hrs
  • Thankx Goodhope Wale wale hana tofauti na flora mbasha ashinde
    Like · Reply · 2 hrs
  • Furaha Mwazembe PESA + MUNGU =PESA MUNGU
    Like · Reply · 2 hrs · Edited
  • Moreen Kowi Kowi Wakupewa Sifa Na Kuabudiwa Ni Mungu Pekee Na Sio Mwanadamu,,kiufupi Bukuku Hakuwa Na Hofu Ya Mungu Kwani Alisahau Pesa Alizohaidiwa Si Chochote Angeweza Kuzipata Mara Kumi Yake Kwa Kufanya Kitu Kingne Tofauti Na Ujinga Huo Ambao Ushakua Upumbavu,
    Like · Reply · 2 hrs
  • Yohana Mwakisole Hakika namuogopa bahat bukuku kwa ujinga huu nitumiwa nyimbo nimeisikiliza mwanzo mwisho. Sasa natangaza yeye pamoja na kazi zake zote sizitaki tena. Kazi zake zote nikifika nyumban naenda kuzichoma.
    Like · Reply · 2 hrs
  • Pius Charles bogus sana
    Like · Reply · 1 hr
  • Geoffrey Mwaswala Hii ndo hasara yakuwa na waimbaji wasiojitambua kama uyo bahat yaan amemsahau Mungu kabisa na kuanza kumtukuza binadam kweli pesa ni habari nyingne
    Like · Reply · 1 hr
  • Maneno Assoly Hiyo ninjaa inamsumbua kamamwezie flora! Inasikitisha sana wanapoteasasa!
    Like · Reply · 1 hr
  • Leah Chrissy Mafwenga Siasa na Mungu ni sawa na mafuta na maji afanye maamuzi aache kusema anamwimbia Mungu atangaze kua mwimbaji wa Lowasa la sivyo itamgharimu
    Like · Reply · 1 hr
  • Leah Chrissy Mafwenga Angeiimba nchi sio mtu kakosea sana
    Like · Reply · 1 hr
  • Petro Byamungu Yohana mwakisole nitumie mmojawapo please whatapp

    0759586272
    ...See More
    Like · Reply · 1 hr
  • Buberwa Mwemezi Changamoto kubwa hii
    Like · Reply · 1 hr
  • Rabson Mahenge Hayo ni maono ya mtu, mbona wewe unakosa kazi yake kwa ushabik wa kisiasa ni nan akuamin wewe kuwa ni mtu mwema na s freemason, yeye kaona bora Lowassa kitu gan kimekukela hadi ukamtoa hadhalan, sisi tunaompenda tutaendelea kununua kazi zake na tutaendelea kumsuport
    Like · Reply · 1 · 1 hr
  • Josephine Kishiwa Tamaa mbaya
    Like · Reply · 1 hr
  • Christina Otieno Ni haki yake kusema yaliyomoyon mwake hata kwa ngonjera au nyimbo,,,
    Like · Reply · 54 mins
  • Paul Mrema yapo mengi yatakayotokea kwa huyu lowasa hilo ni jambo dogo sana kumbukeni shetani ndio ametawala dunia ya sasa sishangai alichofanya huyu bukuku
    Like · Reply · 45 mins
  • Side Shalua Nadhan kila mtu ana rais anayemkubali ivo kila mtu atapiga kura atakayepata nyingi ndio rais
    Like · Reply · 43 mins
  • Makomemanga Cargo Njaa inatisha binafsi nilimkubali sana huyu dada lakini dah ameniangusha kweli mwanamke hafai kuwa imamu
    Like · Reply · 43 mins
  • Paul A Kijuu Ukimwacha Mungu utahangaika sana
    Like · Reply · 39 mins
  • Boniphace Mwambapa Duuu cku za mwisho watu watapenda pesa kuliko kumpenda MUNGU binafsi cjausikia wimbo huo nisiseme chochote mtoa post urushe huo wimbo tuusikie
    Like · Reply · 32 mins
  • Ebardy Robert Ya mungu apewe mungu na yaliyo ya kaisari apewe kaisari,,, amekosa maadili
    Like · Reply · 29 mins
  • Eusebio Mosile hiyi ni hela,inabadilisha kila kitu ukishakubali kutumiwa
    Like · Reply · 29 mins
  • Salumu Mpeni Duh! njaa shidaaaaaaaaaaaaah!!!!!!!
    Like · Reply · 28 mins
  • Issaya Selemani Torongei Mauna Hayo yote nimaneno kama hamna yakusema jama mlale tu
    Like · Reply · 17 mins
  • Sarah William Iyo mwanamke mwenzangu ni njaa
    Like · Reply · 11 mins
  • Rajabu Mkungumika Kiukweli huo wimbo cjausikia hivyo cwezi kuutolea maamuz. Ila bukuku ni mwinjilisti tena ni mwimbaji Gospal. Lakini ktk nyimbo zake sizioni kama ni za mungu zaidi naona kama biashara tu. Hivyo namfananisha yeye kama lady jay dee wa bongo flava. Hivyo kwa mantik hiyo poa ana upeo na haki yake kama w@sanii wengine.
    Like · Reply · 9 mins
    • Owen Mgaya Siku za mwisho ndo hizi
    Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
    Newer Post Older Post Home

    0 comments:

    Post a Comment

    Subscribe to: Post Comments (Atom)

    TOTAL PAGEVIEWS

    Popular Posts

    • LIVE: RAIS MAGUFULI ANAKABIDHIWA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MADINI
    • BREAKING NEWZ: BASI LA NGANGA LATUMBUKIA MTARONI KULIKWEPA LORI
    • THE UDAKUZ: WEMA SEPETU Vs WOLPER!!
    • IRAN NA MAREKANI WAZIDI KUIMARISHA UHUSIANO
    • PICHA YA KWANZA YA KANISA LA ASKOFU MTATA GWAJIMA BAADA YA KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA YA SERIKALI JANA LIVE.
    Copyright © LEMUTUZ

    Developed by MKCT