Tuesday, May 19, 2015



Mh Waziri kabaka kapasua jipu na kuweka wazi kuwa wabunge wawili wa upinzani wamekuwa wakichochea mgomo wa madereva nchini!


Waziri amesema wazi kuwa mbunge mmoja kutoka dares-salaam na mmoja nje ya dares-salaam wa upinzani wamekuwa wakiwasumbua viongozi wa madereva kwa kuwataka waonane nao ili wawambie cha kufanya.


Madereva walichoshwa na usumbufu huo wakaamua kuweka wazi hilo kwa waziri! Waziri amesema wabunge hao wamekuwa wakiwapigia simu viongozi hao ili kuwashawishi kugoma lakini waligonga mwamba maana suluhu ili patikana.


Itakumbukwa kwamba mgomo huu uliwatesa sana watanzania lakini kumbe kuna watu walikuwa wakichochea na wanaendelea kuwa shawishi madereva wakutane nao.

Hawa ndio wakupewa nchi...?


Source:TBC 1(Bunge)

0 comments:

Post a Comment