Filamu hiyo ambayo inadhaminiwa na raia wa Nigeria anayeishi Marekani, Tony Abulu, itahusisha pia wasanii maarufu ambao ni: Tekno, Jide Kosoko, Tina Amuziam, Rachael Oniga, Funnybone, Pencil, Bryan Okwara, Lilian Esoro na wengine.
Abulu, ambaye amekuwa katika tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 30, amekamia kuitangaza zaidi tasnia ya muziki wa Nigeria duniani ili kuipa umaarufu kama wa tasnia ya filamu ya Nigeria ambayo hujulikana kama Nollywood.
Filamu nyingine za Abulu katika tasnia hiyo ni pamoja na ‘Doctor Bello’, ‘Back To Africa’ na ‘Crazy Like a Fox’.
0 comments:
Post a Comment