KUFUATIA
mashabiki kumlaumu kwa kitendo chake cha kuhudhuria shoo ya Zari All
White Party, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja amefunguka kwa ukali
kuwataka watu kumuacha na maisha yake kwa sababu hayawahusu.
Akipiga
stori na gazeti hili, Kajala alisema amekuwa mvumilivu kwa muda mrefu
lakini kitendo cha watu kutaka kumpangia nini cha kufanya au wapi pa
kwenda, kimevuka mipaka maana hawajui alipotoka wala anakokwenda.
“Watu wanazidi sasa, wanataka kunipangia wapi pa kwenda na wapi siyo pa kwenda, kwani kwenda kwa Zari kuna tatizo gani, kwa hiyo mtu akiwa na tofauti na Wema, kila mmoja lazima atofautiane na huyo mtu? hayo mambo ya wapi jamani, watu wasinipangie maisha ya kuishi,” alisema Kajala.

0 comments:
Post a Comment