Posted by Williammalecela.com on Friday, May 01, 2015
Mkewa
staa wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu, Salma Sadiki akiwa na mizigo
yake. Akizungumza na mapaparazi wetu, Salma alisema kwa kipindi kirefu
msanii huyo amekuwa akimuonyesha tabia za ajabu ikiwemo hivi karibuni
kunaswa akiwa amezungukwa na vimwana kana kwamba si mume wa mtu.“Mara
nyingi akiwa anatoka kwenye shughuli za usiku huwa tunatoka wote lakini
cha ajabu kuna siku alinigomea kabisa kwenda naye kwenye lile onesho la
Twanga Pepeta, akarudi saa 11 alfajiri na kwenye bethidei ya mtoto wa
Davina akaniambia mimi nibaki nyumbani kumbe alikuwa ana mambo yake huko
kwani alirudi asubuhi saa 12.Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
KIMENUKA! MKEwa staa wa sinema za
Kibongo, Jimmy Mafufu, Salma Sadiki amenaswa akifungasha virago nyumbani
kwake Mwananyamala-Hospitali na kuelekea kwa wazazi wake maeneo ya
Mbagala jijini Dar akidai kuchoshwa na tabia za mumewe huyo, Ijumaa lina
‘full’ stori.
Siku
ya harusi yao. “Nimevumilia mengi sana kwenye hii ndoa mpaka leo kuamua
kuondoka. Acha nimuache na mambo yake,” alisema Salma kwa
masikitiko.Alisema japo katika uhusiano wao wana miaka isiyopungua saba,
walikuwa kwenye uchumba kwa miaka minne na baadaye wakafunga ndoa mwaka
2013 lakini anashindwa kukumbuka alipotoka.
Baada ya kushuhudia
Salma akiondoka nyumbani hapo, mapaparazi wetu walimtafuta Jimmy kwa
njia ya simu ili kumsikia anazungumziaje madai ya mkewe ambapo alisema
mkewe huyo amekuwa akimuonea wivu usiokuwa na maana.
Mafufu
akiwa na warembo. “Mke wangu nampenda sana na tangu nimuoe sijawahi
kumsaliti sema tu anakosa imani kwa mambo madogo sana. Kama mwenyewe
kaamua kuondoka kutokana na wivu wake mimi siwezi kumfuata,” alisema
Mafufu.
0 comments:
Post a Comment