ILIANZA kama
utani lakini siku zilivyosonga ndivyo uhusiano wao ulivyowekwa wazi,
hao ni watu wawili waliowahi kuwa maadui wakubwa miaka kadhaa nyuma.
Staa wa filamu Shamsa Ford na msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ wakifanya yao.
Hapo
nawazungumzia staa wa filamu Shamsa Ford na msanii wa Bongo Fleva,
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambao kwa sasa wamezama kwenye mahaba
niue.
Awali,
wahusika wote walitumia nguvu kubwa kukanusha juu ya uhusiano wao
lakini inatajwa kuwa mahaba yao ndiyo gumzo kuliko ya wengine wote
katika Bongo Muvi na yanashika nafasi ya pili katika Bongo Fleva nyuma
ya Diamond na Zari kwa sasa.
Awali,
uadui wao ulitokana na Nay kuwaponda wasanii wa kike wa Bongo Muvi na
kudai wengi wao hawana lolote na kazi yao ni kujiuza, Shamsa alikuwa
mmoja wa waliopokea kwa hasira kali na kumbwatukia Nay lakini ule usemi
kuwa ‘wagombano ndiyo wapatanao’, ulikuwa unawahusu.
Sasa inavyoonekana filamu yao imekuwa ya ukweli badala ya
zile za kuigiza. Pichani ni jinsi mahaba nigaragaze yalivyotawala katika
maisha ya wawili hao.
0 comments:
Post a Comment