Monday, May 11, 2015


Mwigizaji na Mwanamuziki Christina Millian akiwa na mpenzi wake Lil Wayne.
Los Angeles, Marekani
Mwigizaji na Mwanamuziki Christina Millian na Lil Wayne wameanzisha mtindo wa kumwagiana sifa kila siku kupitia mtandao, hali inayoelezwa ni kukolea kwa penzi kati yao.


Akizungumza na tovuti ya Perezhilton, Millian alimmwagia sifa mpenzi wake Wayne kwa kusema kuwa ndiye anayemtia moyo katika utendaji wake wa kazi na kumfanya ajihisi mwenye bahati kwa kuwa na uhusiano na kijana huyo. "Kinachonitia moyo na kuniongezea hamasa ya kumpenda, hasikilizi watu wanasema nini juu yangu," alisema Millian.

0 comments:

Post a Comment