Tuesday, May 12, 2015


Mwanamuziki DNA akiwapagawisha mashabiki wa muziki ndani ya Ukumbi wa Jembe ni Jembe, Mwanza.
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Kenrazy akiwa stejini kuwapa burudani mashabiki wa Jembe ni Jembe.


Mwanadada Jokate Mwegelo akiwapa hi mashabiki.
Burudani zikiwa zimepamba moto ndani ya Jembe ni Jembe.
Dada huyu akichana ngoma ya Dumbala ya msanii DNA.
DNA akizidi kuwadatisha mashabiki wake.
Na Johnson James, Mwanza
WASANII wakali kutoka nchini Kenya wakiwemo DNA, Kenrazy, Meja na wengine kutoka Kundi la Grandpa Family usiku wa kuamkia leo wamelitikisa vilivyo Jiji la Mwanza baada ya kushusha burudani ya nguvu kwa mashabiki wao waliofurika kwenye Viwanja vya Jembe ni Jembe.
Msanii DNA ndiye alianza kulipanda jukwaani huku akishangiliwa na mamia ya mashabiki waliofurika katika ukumbi huo wa Jembe ni Jembe kutazama shoo hiyo.
DNA aliwarusha mashabiki wake kwa nyimbo zake mbalimbali kama Fimbo inachapa, Maswali mengi, Dumbala na nyingine kibao jambo lililomfanya ashangiliwe kila alipotaka kupafomu nyimbo nyingine.
Mbali na DNA naye msanii mkongwe wa nchini Kenya, Kanrazy alipanda jukwaani na kuanza kuwaburudisha mashabiki na ngoma zake kalio ikiwemo ile isiyochuja ya Tichi.
Katika burudani hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka, mashabiki walimshuhudia mrembo na mwanamitindo Jokate Mwengelo alipanda jukwaani kuwapa hi mashabiki wake.

0 comments:

Post a Comment