Akizungumza na Nipashe jana mchana kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 5:30 asubuhi huko katika mtaa wa furaha store mbinga mjini.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa kibasa alimfanyia kitendo hicho cha kinyama mwendesha bodaboda Ndunguru alifuatwa na mtuhumiwa kwenye eneo lake la kazi kasha kumkamata na kumpeleka nyumbani kwake ambako inadaiwa alimfunga kamba mikononi na kuanza kumpiga kwa kutumia mkanda wake wa suruali.
Alieleza zaidi kuwa Ndunguru baada ya kushushiwa kipigo na kibasa alibebwa na mtuhumiwa huku akiwa amefungwa kamba mikononi na kumpeleka hadi chooni ambako alimvua suruali aliyokuwa amevaa kisha kumfanyia kitendo hicho cha kinyama huku akielezwa kuwa kwa kuwa umeshindwa kulipa deni lazima ufanyiwe kitendo hicho.
Hata hivyo kamanda msikhela alisema kuwa jeshi la polisi mkoani humo bado linaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo sambamba na kupata ushahidi wa kitaalamu toka kwa madaktari na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.TEMBELEA BLOG YETU KWA HAB
0 comments:
Post a Comment