Erick Evarist STAA wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameacha aibu ya aina yake barani Ulaya baada ya gauni lake kuvuka na kuacha ‘nido’ zake hadharani, Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.
Kwa mujibu wa chanzo, akiwa jukwaani, Shilole alipandwa na mzuka wa aina yake wakati akitumbuiza nyimbo zake kali ndipo nguo zake zilipojiachia na kusababisha nido zake kuonekana, hali iliyowapa mhemko wa namna yake wanaume waliohudhuria shoo hiyo.
“Ishu ilikuwa hivi, mimi nilikuwa kwenye mzuka wa shoo, kuna mtu ambaye alikuwa ananifuatilia tu kila ninalofanya jukwaani ili aniharibie kwa sababu hakufurahishwa na mimi kufanya shoo na Manganga One (muandaaji)
“Alichokifanya yeye ni kuniwinda pale bahati mbaya braa iliposhuka kutokana na mishemishe za kucheza, akapiga picha hiyo kisha akaiweka mitandaoni ili kunikomoa,” alisema Shilole.
Alipoulizwa sababu za mtu huyo kumtegea picha hiyo, Shilole alisema alimkatalia kufanya shoo yake kwa kumueleza kuwa hawezi kufanya shoo yake kabla hajamalizana na Manganga One ambaye ndiye alikuwa amewahi kuomba huduma yake.
0 comments:
Post a Comment