AIBU!
Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Joseph amejikuta akiaibika
vikali kufuatia kudaiwa kunaswa akiwa na mwanamke mwingine ilhali yeye
ni mume wa mwanamke aitwaye Sophia, Amani limenyetishiwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, aibu hiyo ilimkuta Joseph, kwenye Kitongoji cha Nyihongo wilayani
Kahama, Shinyanga .
Mashuhuda
waliliambia Amani kwamba, Joseph ni fundi ujenzi na siku ya tukio
alinaswa kwenye nyumba inayojengwa na yeye lakini ikiwa bado
kumalizika.“Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake
lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye
alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.
...Wakizidi kumpa kichapo.
“Sasa siku ya tukio, Jose alionwa
na mtu mmoja akiingia kwenye nyumba inayojengwa. Yule mtu alishajua
Jose anachepuka na yule mke wa jamaa, akaenda kumwambia ndiyo wakamzukia
na kumnasa,” kilisema chanzo.
Chanzo kikaendelea kuweka wazi
kuwa, baada ya Jose kunaswa alitembezewa kichapo kizito na kupelekwa
kwenye ofisi za serikali ya mtaa ambapo Jose alipigwa faini ya shilingi
laki tatu.
“Lakini kilichotokea sasa ni
kwamba, baada ya kulipa faini hiyo, mke wa Jose naye kwa hasira aliamua
kuondoka nyumbani na kwenda kwao.
Mke wa aliyefumaniwa.
“Alisema amelazimika kuondoka kwa
Jose kwa sababu kitendo alichokifanya kimemtia aibu kubwa. Kwamba
haiwezekani yeye atulie nyumbani Siku ya Wapendanao halafu mumewe
akachepuke mitaani na mwanamke mwingine,” kilisema chanzo
0 comments:
Post a Comment