Posted by Williammalecela.com on Saturday, May 30, 2015
C
KIMENUKA! Ikiwa ni siku moja tu kabla ya kufungwa kwa ndoa kati ya
Zuhura Omari na Abdallah Salehe, katika hali isiyotarajiwa, mke
mtarajiwa amekataa kushiriki tendo hilo la kheri licha ya taratibu zote
kukamilika na kusababisha tafrani kubwa huko Buguruni Kwa Mnyamani
jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ndugu
wakiwa hawana la kufanya baada ya binti huyo kugoma kuolewa. Tukio hilo
lilitokea Mei 23, mwaka huu wakati ndugu wa mume walipokusanyika
nyumbani kwa Abdallah tayari kwa shughuli, lakini wakalazimika kuondoka
baada ya kuelezwa kuwa mwanamke amekataa kuolewa, ikidaiwa ni mara ya
pili baada ya kufanya hivyo tena mwaka jana.
Shuhuda wa tukio hilo
aliliambia Ijumaa kuwa baada ya kukataa mwaka jana, taratibu nyingine
zote, ikiwa ni pamoja na mahari na zawadi ndogondogo zilipelekwa ukweni
na ndoa hiyo ikapangwa kufungwa Mei 22, mwaka huu, lakini ghafla
wakapata taarifa hizo za kushangaza.
Akizungumza na gazeti hili,
mdogo wa mume mtarajiwa ambaye alipewa jukumu la kumwakilisha kaka yake
kwenda kumchukua mke, aliyefahamika kwa jina la Salehe alisema hadi siku
hiyo, walikuwa wameingia hasara kubwa, hivyo kutaka walipwe gharama
zote walizotoa, ikiwemo mahari (450,000), kitanda, godoro, kabati na
magunia ya mchele uliokuwa upikwe shughulini.
Mmoja
wa wanafamilia wa bwana harusi. Waandishi wetu waliokuwa eneo la tukio
waliwashuhudia baadhi ya mawifi wakiwa katika sare zao za madela
wakingojea muafaka wa harusi hiyo huku wengine wakiandamana hadi
nyumbani kwa bibi harusi wakidai ufafanuzi zaidi.
Bi harusi ambaye
aliomba asipigwe picha alikiri kuwa ni mchumba wa Abdallah kwa mwaka
mmoja na alitakiwa aolewe Mei 23, mwaka huu, lakini aliamua kubadili
msimamo akidai mchumba wake ni mtata kwani amekuwa akimtuhumu kutembea
na mpemba mmoja (jina halikupatikana).
“Huyo Mpemba nilisoma naye sekondari, kwa sasa ni rafiki yangu wa kawaida. Nimegoma kuolewa kwa sababu mwanaume ni mtata sana.
Mmoja
wa wanafamilia akiwasiliana kwa simu. Binafsi nimeshindwa kwa sababu
malengo yangu siyo niolewe leo halafu kesho nirudi nyumbani, nataka
nikae na familia, tuzae tukiwa na amani na mume wangu, ila kwa huyu
nimeshindwa, kama wameandaa pilau lao huko lidode tu,” alisema Zuhura
huku mama yake akidai wamesharudisha baadhi ya vitu walivyopewa.
Jitihada za kuzungumza na bwana harusi hazikuzaa matunda ila jitihada za kumtafuta zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment