Saturday, May 23, 2015

WALIO LOGA WASHINDA MAGOLI SITA


Kocha wa timu ya Lukili FC mkoani Geita Seleman Shabani na nahodha wa timu hiyo Lucas James wanyakwa usiku wa saa tano na dakika ishirini wakitimiza masharti ya benchi la ufundi.Tukio hili lilitokea mkoani Manyara.


Mauza uza hayo yalifanyika uwanjani JK Nyerere stadium nakunaswa live na walinzi wa uwanja huo.Wamedai walikua wanasafisha uwanja kukwepa dhoruba ya magoli.Lukirini FC kutokana na ndumba waliibuka na magoli sita dhidi ya Mtwivila City ya Iringa iliambulia goli moja la kufutia machozi.


Ikumbukwe soka la bongo limekua likishuka kutokana na imani za kishirikina zaidi kuliko kufanya mazoezi na kutumia akili ya mpira,soko la Tanzania linaitaji mabadiliko makubwa kufikia mafanikio.

1 comment:

  1. Tunasema kila siku hapa kuwa soka la bongo ni la miujiza. We angalia wachezaji wetu wa simba na Yanga, wanavyocheza mpira mchangani halafu uambiwe huyu anachezea simba ama Yanga utabisha, cha kushangaza mchezaji huyo huyo anatuwakilisha kwenye taifa stars, tutegemee nini? Soka ni kipaji si ndumba.

    ReplyDelete