Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Roland Coulon (Kushoto) akiongea Machache wakati wa Uzinduzi wa Huduma Mpya ya Benki hiyo Ijulikanayo kama kwa jina la "RAHISI".
Huduma hiyo inawawezesha Wateja wa Access Benki kupata huduma Kwanjia ya Simu ya Mkononi Access benki Wamezindua huduma hiyo kwa Kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Selcom Tanzania Kushoto Ni Huduma rahisi inayowawezesha wateja kufanya mihamala Popote na bila malipo yoyote,kulia Ni Meneja masoko wa Access Benki Ndugu Jonas Muganyizi.
Mkurugenzi wa Idara ya benki bila tawi na Maendeleo ya Biashara wa access Benki Ndugu Andrea Ottina akielezea namna Faida za kutumia Huduma yao waliozindua Leo Ijulikanayo kama "RAHISI" na Usalama wakati wa Kutumia huduma hiyo.Alisema huduma hiyo ni Rahisi sana kuitumia na Pia ina usalama wa hali ya juu hivyo wateja wasiwe na wasiwasi wowowte mihamala watakayofanya itakuwa salama.Akieleza Zaidi Mkurugenzi Mtendaji alisema mteja anaweza kufanya Mihamala Muda wowote na Pia wateja wanaweza kufanya miamala Mingi zaidi bila kikomo
.
.
Meneja masoko wa Access Benki Ndugu Jonas Muganyizi akieleza zaidi kuhusu huduma hiyo.



0 comments:
Post a Comment