Mwanamama
mjasiriamali, na managing director wa jarida maarufu nchini , Bang
magazine , aitwaye Emelda Mwamanga amefunguka kuhusu bifu lake na
mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, kupitia kwenye moja ya
mahojiano ya kwenye kipindi maarufu cha Tv Hapa nchini .
Mbali
na kuelezea experience yake kwenye biashara yake, pia alizungumzia
changamoto mbali mbali anazokabiliana nazo kwenye biashara zake, moja ya
changamoto alizozielezea ni ile ya kushtakiwa na mfanyabiashara maarufu
nchini, Reginald Mengi, ambaye ni mume wa aliyekuwa miss Tanzania,
Jackline Ntuyabaliwe maarufu kama K-Lyn.
Akielezea
chanzo cha kushtakiwa, mwenyewe anadai ni kuvujishwa kwa picha za
mfanyabiashara huyo akiwa na familia yake, kitendo ambacho
mfanyabiashara huyo hakukipenda hivyo aliamua kumshtaki mwanamama huyo
kama adhabu na fundisho.
Akielezea
kwa masikitiko mwanamama huyo alielezea jinsi ya picha hizo
zilivyosambaa mitandaoni, ambazo zilipigwa mahsusi kwa ajili ya kupambwa
kwenye jarida maarufu la mwanamama huyo, hata hivyo inasemekana baadhi
ya wahariri wa jarida hilo walizivujisha picha za Mengi huyo kwenye
mitandao ya kijamii either kwa bahati mbaya au kwa kukusudia , kitendo
kilichomkera Mengi na kuamua kumshtaki.

0 comments:
Post a Comment