Thursday, June 4, 2015

Mapema wikitulikuletea stori ya ajali ya lori la mafuta kuua zaidi ya watu 90 huko Nigeria ikiwa ni baada ya kuwa kwenye mwendo mkali na kuginga watu na magari yaliyokuwa kwenye kituo abiria.
Muonekano wa kituo cha mafuta baada ya kulipuka
Lakini leo Ghana nayo imeingia kwenye headlines baada ya kituo cha mafuta kulipuka na kuua watu wanaokadiriwa kuzidi 90 katika mji mkuu wa nchi hiyo Accra.
Mlipuko huo umetokea baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya mji huyo ambapo pia imewaacha watu wengi bila makazi huku sehemu kubwa ya mji ikiwa haina gizani kutokana na kukatika kwa umeme.
Mwili wa mtoto ukiokotwa katika eneo la kituo hicho
Inasemekana watu wengi wamepoteza maisha baada ya kuwepo kituoni hapo wakijikinga na mafuriko yaliyotokea na huenda idadi ikaongezeka kutokana na baadhi ya miili kuwa bado haijapatikana.

0 comments:

Post a Comment