Wachezaji na makocha wa Mwadui FC wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa makiendesha kuelekea Shinyanga kupata ajali na kupinduka mara tano kabla ya kusimama.
Wachezaji hao wakiwa na makocha Habib Kondo na Khalid ( kocha wa makipa) walikuwa njiani kwenda kujiunga na kambi ya timu yao ya Mwadui FC.
“Sababu ya gari kupinduka ilikuwa ni baada ya tairi la nyuma kuchomoka,baada ya hapo gari ilipinduka karibia mara tano,hatukuumia sana isipokuwa mimi tu nilipata michubuko kwenye mkono”, Shabani Kado ameuambia mtandao huu
0 comments:
Post a Comment