Kuna kila dalili kuwa katibu wa Wiaya ya Kibaha Vijijini ni Team Fulani . Kitendo cha kukimbia kinaonesha ametumwa kufanya hivyo, na amekubali kutekeleza jambo la kijinga kiasi hicho, jambo ambalo ni la kukidhalilisha Chama Cha Mapinduzi mbele ya watanzania na mbele ya wanachama wake maelfu waliojitokeza kumdhamini mwanachama mwenzao.
Kama angekuwa na hekima kama ana shughuli yake muhimu mahali fulani angejieleza na isingeshindikana kumfuata aje mara moja kutekeleza wajibu wake na kumrudisha kwani tukio hilo ni la dakika chache na si saa kadhaa. Chama Cha mapinduzi kinahitaji kuachana na watendaji na viongozi wenye tabia ya aina hii




0 comments:
Post a Comment