Taarifa kamili ya Ajali iliyotokea hapa MBINGA ni kama ifuatavyo, mnamo tarehe 04.06.2015 Majira ya saa kumi jioni gari T.306 AYM L/Rover 110 wagon ikiendeshwa na padre Yasint Yasint KAWONGA ilishindwa Kupanda mlima ikarudi nyuma na kudondokea kwenye kijimto kisichokuwa na Maji kisha gari hiyo kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu saba, wanawake wawili na wanaume watano akiwemo dereva father KAWONGA, majeruhi ni 24 walio serious sana ni wanne wamelazwa Hospt ya Mbuyula-mbinga wanaume watatu mwanamke mmoja. Marehemu na majeruhi wote ni wanafunzi kidato cha Pili na NNE, CTC Sec School inayomilikiwa na huyo padre Dereva aliyefariki. Gari hiyo ilijaza sana wanafunzi walijaa ndani ya gari na wengine walining'inia nje ya gari wengine ktk boneti wengine juu ya carrier ya gari, jumla kwenye gari hiyo walikuwa wanafunzi thelethini. Nawasilisha Tafadhali Usk mwema wapendwa
0 comments:
Post a Comment