Wednesday, June 3, 2015

KWAKO supastaa usiye na mpinzani Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, habari za siku kaka? Pole kwa mishemishe na harakati za muziki wako.Ukitaka kujua hali yangu, mimi ni mzima wa afya. Namshukuru Mungu kwa kunijalia uzima, naendelea kupambana na maisha kama kawa. 
Dhumuni la barua hii kwanza ni kutaka kuzungumza na wewe kuhusiana na suala zima la kuwasomesha watoto ambao mwaka jana uliahidi kuwalipia ada katika Shule ya East Africa International jijini Dar.Kwanza nikupongeze kwa wazo lile. Lilikuwa zuri mno, hakuna muungwana yeyote anayeweza kubeza wazo hilo hata kidogo. Binafsi nilifurahi kwani nilijua umetambua umuhimu wa kurudisha fadhila kwa jamii.  

0 comments:

Post a Comment