Monday, June 15, 2015


Vigezo na sifa nane mahsusi kwa mtanzania anayetaka kugombea urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo (kama zilivyopitisgwa na Kikao cha Halmashauri Kuu Mjini Tabora-Tarehe 13 Juni 2015).


i) Awe ni mtu anayejitegemea kutokana na chanzo halali cha kipato
 

ii) Awe tayari kutangaza mali binafsi na vyanzo vyake kwa kufuata utaratibu ulioanishwa katika Sehemu ya VI ya Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya ACT-Wazalendo
 

iii) Awe ni mtu aliyethibitika kuielewa itikadi, falsafa, misingi na sera za ACT-Wazalendo na aonyeshe utayari wa kuisimamia na kuiishi
 

iv) Awe ni mtu anayeonyesha kuyaelewa matatizo ya Tanzania ya sasa na ya muda mrefu, na mwenye maono mapana juu ya maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya kizazi kijacho
 

v) Awe ni mtu anayeonyesha kuwa na upeo mpana kuhusu masuala ya Afrika na ulimwengu katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kijiografia na kijamii
 

vi) Awe ni mtu ambaye ana haiba na taswira ya kuiwakilisha na kuipa heshima stahiki Tanzania katika Jumuiya ya Kimataifa
 

vii) Awe ni mtu ambaye ana nia ya dhati ya kulinda na kusimamia bila kuyumba Muungano wa Tanzania
 

viii) Awe ni mtu ambaye anaguswa na umaskini wa watanzania wa vijijini na kuonyesha utayari wa kusimamia sera pendeleo kwa ajili ya wananchi waishio vijijini kama ambavyo Azimio la Tabora limenuia

0 comments:

Post a Comment