Wednesday, June 17, 2015

Hivi ndivyo mchakato wa kuwachuja wagombea ndani ya chama cha mapinduzi utakavyokuwa.

1. Kamati ya Maadili ya CCM, ambayo inaongozwa na Mzee Mangula itakaa na kuwajadili watia nia wote wa CCM na kuwapatia alama i.e A,B,C,D & F. Pamoja na kuwapatia alama pia Kamati ya maadili ya CCM itawa rank watia nia wote in priority order. 1,2,3,4,5.................... 35(?). Kamati ya maadili itapeleka majina ya watia nia wote na alama zao na ranking zao kwenye kamati kuu ya CCM.


2. Kamati Kuu ya CCM itakaa na kupitia na kujadili majina ya watia nia wote. Kamati kuu ya CCM itapendekeza majina yasiyozidi matano kwenda NEC kwaajili ya kupigiwa kura.

3. NEC itapigia kura majina 5 yaliyoletwa na Kamati kuu ya CCM na majina matatu ya kwanza yatapelekwa Mkutano Mkuu kwaajili ya kupigiwa kura.

4. Mkutano Mkuu wa CCM utapigia kura majina 3 yaliyotoka NEC na jina litakalopata >50% ya kura za wajumbe wa mkutano mkuu ndiye atakuwa mgombea wa CCM.

4 (ii) Kama katika duru ya kwanza ya upigaji kura kwenye mkutano mkuu, kutakuwa hakuna mgombea/jina litakalopata >50%. Basi majina mawili ya kwanza yataingia katika duru la pili la kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu. Jina litakaloshinda kura katika uchaguzi wa duru la pili, ndiye atakuwa mgombea wa CCM.

0 comments:

Post a Comment