NAIBU Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba ambaye ni mmoja wa makada wa CCM waliotangaza nia ya kuwania kuteuliwa kuwania Urais, ameibuka na ubunifu wa kisasa katika namna ya kutangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, kitu ambacho endapo kitafanikiwa atakuwa amemfunika Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa ndiye gumzo miongoni mwa makada waliojitokeza.
Licha ya kuonekana katika skrini hizo, watu wangepa fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo kutoka popote walipo.
Gazeti hili lilikuwa limeshakwenda mitamboni kabla mwanasiasa huyo hajatangaza nia yake.
Kabla ya ubunifu huo, Lowassa alikuwa akishikilia rekodi ya tukio lake la kutangaza nia kwa kujaza watu wengi uwanjani huku maelfu wakifuatilia katika vituo vya televisheni tukio hilo lililofanyika Mei 30, jijini Arusha.
0 comments:
Post a Comment