Mke wangu Ramona sio mwanasiasa wa jukwaani. Ni nadra kwake kuzungumza na hadhara. Lakini katika wiki mbili hizi, nimeshangazwa na umahiri wake jukwaani. Amekuwa akishiriki na wakati mwingine kuzungumza katika mikutano yetu na wana-CCM ya kutafuta udhamini nchi nzima. Namshukuru sana Mke wangu, pamoja na watoto wetu wawili, kwa uvumilivu na upendo, na kwa kuelewa kwamba maisha yangu yamekuwa ni maisha ya watu wote. Ni maisha ya kutoa huduma kwa jamii, na kwamba familia yetu ni zaidi ya yeye na mimi pamoja na watoto wetu, bali ni familia pana zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment