Sunday, June 28, 2015

Mh January Makamba Jana baada ya Kumaliza Singinda alielekea Mkoa wa Manyara, Babati kuomba udhamini na kuzungumza na Wanachama pamoja na Wakazi wa Babati juu ya dhamila yake ya kuomba nafasi ya kuongoza Tanzania.
Mh January alipokelewa vizuri sana na wakazi Babati na akapewa udhamini wa kutosha. January makamba akizungumza na wanababati alisema kuwa Urais sio kama Ngoma ya Mdundiko unaingia na kuifaita unapofika mbele unajikuta haujui umefikaje na haujui jinsi ya kurudi, kabla ya kuomba nafasi hiyo inabidi ujiulize maswali katika nafsi yako na ujilishe kuwa unaweza, kwanza ujiuliza je unamajawabu mapya ya kutatua changamoto za watanzania?
Vijana wa Bodaboda Babati waliojitokeza kumpokea Mh January Makamba wakiwa katika msafala kuelekea Ofisi za CCM Babati.

Mh January Makamba akisalimiana na wakazi pamoja na wanachama wa CCM waliojitokeza kumsikiliza Babati.


Shekhe akitoa dua kabla ya zoezi zima la Mh January Makamba kuzungumza na wakazi wa Babati


Askof Pia akitoa neno na kumuombea January Makamba katika safari yake ya kutaka kuiongoza Tanzania.


Mh January Makamba akivishwa Shuka na moja ya Mzee wa Babati kwa mira pamoja na desturi za Babati 












Mh January Makamba akimtambulisha Mke wake kwa wakazi wa Babati.





0 comments:

Post a Comment