Friday, June 26, 2015

MKALI wa filamu za kibongo Jacop Stephen ‘JB’, amefunguka kuwa kazi zao zimekuwa zikikubalika sana na Watanzania lakini anashindwa kuelewa ni kwa nini bado baadhi ya wasanii wanaishi maisha mangumu.
JB ambaye anaonekana kufanya vizuri kwenye tasnia hiyo, amesema bado wanachangamoto nyingi za kuangalia namna na kujikwamua na hali ya umasikini kwa wasanii wa Tanzania.
“Ni lazima tukubali kupapambana maharamia ambao wanatufanya sisi wasanii kuwa na majina makubwa lakini hatuna hela, kazi zetu zipo kila kona ya Tanzania zinatazamwa lakini unakuta msanii huyo huyo maisha yake yanakuwa mabovu wakati mauzo ya kazi zake yanaonekana kuwa juu,” alisema”.

0 comments:

Post a Comment