Saturday, June 6, 2015

Habari kutoka wilaya ya Songea mkoani Ruvuma zinasema kuwa kumeibuka kikundi cha kihalifu cha wapiga nondo na wakata mapanga ambao pia wamekuwa wakipora pikipiki na mali mbalimbali.
Hata hivyo jeshi la polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa wa kikundi hicho na mali kadhaa za wizi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela amesema mali kadhaa za wizi zimekamatwa zikiwemo simu,Deki na Tv.
Kamanda Msikhela amesema kuwa wahalifu hao wamekuwa wakitumia nondo,mapanga kisha kuvamia watu na kufanya uporaji wa mali zikiwemo pikipiki na kwamba watu tisa wanashikiliwa kwa uhalifu huo.

Via>>ITV

0 comments:

Post a Comment