OMARY
Faraji Nyembo, anayefahamika zaidi kimuziki kama Ommy Dimpoz ni msanii
mwenye jina kubwa katika fani, ingawa ni miongoni mwa vijana
waliochipukia na kupata umaarufu katika miaka ya hivi karibuni.
Amefanya
kazi nyingi nzuri na zilizopata kupigwa sana katika vituo vingi vya
redio na televisheni, baadhi yake vikiwa ni pamoja na Baadae, Me and
You, Ndagushima na Wanjera, kitu kinachomfanya kuwa miongoni mwa wasanii
wanaofanya vizuri katika soko la Bongo Fleva kwa sasa.
Ingawa
hatambi sana, lakini uwezo na kazi zake kwa sasa unamfanya kuwa mmoja wa
wasanii ambao kukosekana kwake katika shughuli yoyote kubwa ya burudani
ni kero kwa mashabiki. Anategemewa kuwepo miongoni mwa vijana kumi bora
wa muziki wa kizazi kipya.
Kwa upande wake, Martin Kadinda ni
miongoni mwa wabunifu vijana wa mavazi hapa nchini, ingawa fani hii
haimpi jina sana kama ile ya kuwa meneja wa muigizaji Wema Sepetu.
Lakini kiukweli, Martin yupo sana kwenye ubunifu na mitindo.
Nimemfahamu
kitambo kidogo, akishiriki kupanda jukwaani kusindikiza nguo
zilizobuniwa naye au ‘dada zake’ Khadija Mwanamboka na Asia Idarous au
wabunifu wenzake akina Ally Rhemtulah.
.
0 comments:
Post a Comment