Thursday, June 4, 2015

Wageni wa Makongoro Nyerere waliotoka Visiwani Zanzibar.

Balozi Amina Salumu Ali akionesha fomu ya Urais mara baada ya kukabidhiwa makao makuu yachama cha Mapinduzi Dodoma.
Mbunge wa Afrika Mahariki Makongoro Nyerere akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa fomu katika ukumbi wa CCM Dodoma leo.
Balozi Amina Salum Ali pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere leo wamechukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi katika kinyanga’anyiro kitachofikia tamati mwezi oktoba mwaka 2015.
Akizungumza mara baada ya kupokea fomu hiyo ya Urais Amina Salum amesema kwamba anaomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi huku kauli mbiu yake ni matumaini mapya kwa kizazi kipya na kuahidi kutowaangusha watanzania kwani wanawake wamekuwa na historia ya kutohusika na ufisadi pamoja na utendaji wenye tija.
Kwa upande wake Makongoro Nyerere amesema kwamba akipata nafasi ya kuwa rais wa Tanzania ata hakikisha kuwa ana pambana na ufisadi pamoja na mafisadi kwa kuwa serikali imeshindwa kuwashughulikia kwa kuwa na majina makubwa serikalini.
Leo wanasiasa wanne wamechukua fomu ya kugombea urais ambapo ratiba inaendelea tena siku ya kesho kwa wanasiasa takribani watano wengine kuchukua fomu.

0 comments:

Post a Comment