Mbunge
wa Mbeya Mjini Mh Joseph Mbilinyi "Sugu" ameamua kulitolea ufafanuzi
bungeni suala la kumpeleka mahakamani Mzazi mwenzie ili apewe ridhaa ya
kumlea mtoto wao, na hilo limetokana na kujibu kauli ya mbunge Martha
Mlata aliyoitoa bungeni jana kuwa kampora mtoto huyo kutoka kwa mama
yake
Mh
Sugu ameitoa kauli hiyo leo hii Majira ya Saa sita mchana na kusema
kuwa anashangazwa na kusikitishwa na kitendo cha Mbunge Martha Mlata
kuongelea suala hilo hadharani tena ndani ya ukumbi wa bunge, na kusema
yapo mambo ya siri ambayo mtu asingependa yazungumzwe hadharani hasa
yale ya mahusiano
"Mh
Naibu spika nasikitika sana kwa kitendo hicho cha mbunge Mlata
kuzungumzia mambo yangu, lakini hazungumzii ya kwakwe yaliyopelekea ndoa
yake kuvunjika, na amekuwa akijitangaza kuwa yeye ni mlokole, sasa ni
ulokole upi unakubaliana na mtu anayekiuka maadili kwa kuvaa mavazi
yasiyo na maadili ya kitanzania" amesema Sugu
Amesema
aliamua kwenda mahakamani kuomba ridhaa ya kumchukua mtoto ili amlee
baada ya kuona mzazi mwenzie kuwa hana maadili na amekuwa akivaa nusu
uchi na picha zake kusambaa mitandaoni ikiwemo inayomuonesha akiwa
amevaa pampasi na nyingine zikimuonesha akiwa amevaa mavazi yanayoonesha
nyeti zake picha zilizopigwa kwenye utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Music
Awards 2015
Amesema
kabla ya Martha Mlata kurusha shutuma dhidi yake ni vema angemfuata na
kumwambia ili Mh Sugu ampe vithibitisho kabla ya kuweka mambo yake
hadharani tena buungeni
Katika
hatua nyingine Sugu ameweka wazi kuwa pamoja na mahakama kumpa kibali
cha kumchukua mtoto wao kwenye himaya ya mama yake, lakini bado
hajamchukua na amesema yeye kama binadamu ameacha suala hilo kwa kuwa
linaendelea kupatiwa ufumbuzi kifamilia
Naye
naibu spika Job Ndugai amewataka wabunge kuacha kuliongelea tena suala
hilo mara baada ya maelezo hayo ya Mbunge Sugu, huku pia akiwaomba
waandishi wa habari kuacha kulikuza suala hilo ili kuepusha kumuathiri
zaidi mtoto wa Mbunge Sugu na Faiza
0 comments:
Post a Comment