Mziwanda amefunguka baada ya msichana Rose John kudai kuwa ana ujauzito wa miezi miwili wa msanii huyo. Msichana huyo alizungumza jana kupitia Uheard na Soud Brown ambapo
alisema kuwa amekuwa na uhusiano na Nuh kwa miaka miwili lakini walitengana baada ya kusikia ana uhusiano na msanii Shilole na kwamba amechora tatuu ya jina lake. Niliachana naye baada ya kusikia nauhusiano na Shilole na pia amechora tatuu ya jina lake lakini tulianza tena
uhusiano miezi miwili iliyopita
niliamua kupima ndiyo nikagundua
nina mimba ya miezi miwili,’’alisema
Rose.
Rose aliongeza kuwa hana mpango wa
kutoa mimba hiyo kwa sababu
anapenda msanii huyo ndiyo maana
ameamua kumzalia.
Kwa mujibu wa msichana huyo
alisema kuwa Shilole na marafiki zake
walimfanyia vurugu na kumdhalilisha
kwa kumpiga kumchania nguo hadi
kupoteza simu na vitu vyake vingine.
Hata hivyo kupitia akaunti yake ya
Instagram Nuh Mziwanda alifunguka
na kumjibu msichana huyo… Ndiyo
mimba ni Jambo la Kheri’ila ni special
na Maalumu kwa nimpendae’na sio
Huyo dada anaetangaza Ana mimba
yangu’na anazidi kutangaza kwenye
vituo vya habari tofauti’mbona
hakutangaza kama Mimi bwana wake
aje kusema Ana mimba yangu’Naomba
mwambie ajipange tena upyaaaa aje
na nyingi be’…
0 comments:
Post a Comment