Friday, June 12, 2015

Mwanamitindo anayetikisa Marekani, Amber Rose.New York, Marekani
MWANAMITINDO anayetikisa Marekani, Amber Rose juzikati alizindua kitabu chake kinachotambulika kama How To Be A Bad Bitch kilichoacha utata katika mitandao ya kijamii kutokana na jina lake.
Kava la kitabu kinachoitwa 'How To Be A Bad Bitch'.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Amber aliachia kava la kitabu hicho kinachotoa somo la jinsi ya kufanikiwa kwenye maisha kilichochapishwa na kusambazwa na Kampuni ya Simon & Schuster Imprint kisha akaambatanisha na maneno yaliyosomeka; “Kitabu changu cha How To Be A Bad Bitch sasa kinapatikana mitandaoni.
Wengi wanajua kuwa Bitch ni mtu malaya lakini niwaambie Bitch ni mpambanaji. Na Bad Bitch ni mtu anayejitambua, anajua anataka nini na mwenye pesa.”

0 comments:

Post a Comment