Wakati Nasibu Abdul ‘Diamond’ akijinadi kwa mbwembwe kuwa anategemea
kiumbe kutoka kwa mwandani wake Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’,
ubuyu mpya wa mjini unadai kuwa mimba aliyobeba mrembo huyo si ya
Diamond, Amani limemeza sababu za kutosha.Kwa mujibu wa chanzo chetu
kilicho karibu na Diamond anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Nana,
tangu habari ya ujauzito wa mlimbwende huyo
mwenye asili ya Uganda ianze kupamba vyombo mbalimbali vya habari, watu walio karibu na staa huyo hawakuziamini. “Hatukuamini sababu kwanza muda ambao Diamond alikutana na Zari ulikuwa mchache ukilinganisha na miezi mitatu ambayo mimba ilibainika. Watu wa karibu tulikuwa tunajua lakini tulikuwa tunashindwa pa kuanzia kusema.“Sijui bwana nani alivujisha hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ndiyo maana hata sisi sasa tukawa radhi kufunguka. Tena imeeleza mambo ya ukweli tupu ambayo sisi tulikuwa tunayajua,” kilisema chanzo chetu.

0 comments:
Post a Comment