Tuesday, June 30, 2015




Dada huyu pichani jana aliandamwa na kuzomewa na baadhi ya wakazi wa Iringa Mjini hususan wanaume wakidai kuwa ametembea nusu uchi. Jambo hili linakanganya; ni nani mwenye mamlaka ya kuamua kama anayetembea barabarani yu nusu uchi au la? Maana, fasheni siku hizi ziko za aina mbali mbali.
Dada huyu amefanya kosa gani? Je, jambo hili lingewezekana kutokea kwenye miji kama Dar ambako si tu huonekana wanaume kwa wanawake wenye kuvaa fasheni mbali mbali za Kimagharibi?




Mbona hawazomewi dada zetu wenye kucheza shoo kwenye steji za muziki wakiwa na ' vichupi'? Na wanaume wenye kutembea vifua wazi na kuvaa suruali nusu matako tuwafanyeje?
Dada aliyezomewa na wanaume ana haki ya kudai kuwa amedhalilishwa kijinsia kama akipeleka kwa hakimu ushahidi wa picha hizo. Katika hili ' Mwenyekiti' wenu naweza ' KujiTunduLisssu' na kusimama mahakamani kumtetea dada yangu huyu. Na namini atashinda na kulipwa fidia!

Na nyie mmesimamia wapi kwenye mkanganyiko huu?

1 comment:

  1. Kwa kweli hawana haki ya kumzomea...huo ni ushamba...hii ni nchi huru.

    ReplyDelete