Posted by Williammalecela.com on Thursday, June 11, 2015
Wema akiwa ndani ya gari hilo. Musa mateja
Ni noma! Kumbe lile gari la kifahari aina ya BMW ambalo muigizaji nyota
wa filamu Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ alizawadiwa wakati wa bethidei yake
na kuwa miongoni mwa sababu za kumwagana na mpenzi wake wa awali, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ mwaka jana, linadaiwa kuwa kimeo kwa vile
limekuwa likiharibika mara kwa mara, Amani lina stori kamili.
Gari
aina ya BMW la Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. Mapema
wiki hii, paparazi wetu alikuta gari hilo likiwa limebuma mitaa ya
Victoria, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku mshindi huyo wa Shindano
la Miss Tanzania mwaka 2006 akiwa ndani, lakini ili kukwepa aibu,
aligoma kutoka nje kuomba msaada, badala yake akabakia ndani huku
akijaribu kuwasiliana na watu wake wa karibu.
0 comments:
Post a Comment