Friday, June 12, 2015

Meneja wa Kilimanjaro ,Pamela Kikuli akizungumza na wanahabari Kuhusu Kilele cha Utoaji wa Tuzo Za Kili Music Awards.Akieleza zaidi Amesema Tuzo za Mwaka Huu zitakuwa za Kipekee na Kwamba kutakuwa na vitu vya Tofauti .Aidha amesema wasanii Mbalimbali wa Hapa Nyumbani watapamba Tuzo hizo
Wanahabari wakichukua tukio.
Washindi  Kili Music Awards 2015 (KTMA) wanatarajiwa kuanikwa kesho ndani ya Ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar. 
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja wa Kilimanjaro, Pamela Kikuli amesema kuwa washindi waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. 

“Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi na jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo washindi hawa wataungana na washindi wengine wanne wa hapa Dar es Salaam,” alisema Kikuli. 

Bi. Pamela aliongeza kuwa washindi hao waliochaguliwa kwa njia ya kuponi baada wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni watalipiwa gharama zote za usafiri, malazi na chakula kwa kipindi cha siku zote tatu watakazo kuwa hapa jijini. 

“ Washindi watakaokuja ni kutoka katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kahama, Musoma na Dar es Salaam.”

0 comments:

Post a Comment