Mwenyekiti wa UV-CCM Taifa Sadifa JUma leo mjini Arusha amewatoa hofu
wfuasi wa msaka urais EL kuwa hakuna mgombea atakaye katwa jina
"kijinga".
Amesema yeye ni mjumbe wa kamati kuu na hatakubali kuona
mgombea mwenye sifa kama EL akikatwa jina kwasababu za kijinga na kwamba
wote wanaomchafua EL ni wajinga na wapumbavu.Kauli hiyo ya Sadifa imewafurahisha sana wafuasi wa EL hasa mwenyekiti wa mkoa wa Arusha Onesmo Nangole.
Sadifa alikuwa anahutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya makumbusho ya azimio la arusha wakati wa kumsimika kamanda wa vijana wilaya ya arumeru Mathias Manga.

0 comments:
Post a Comment