UBABE?
WASANII katika tasnia ya filamu, Irene Paul ‘Smart Girl’ na Halima
Yahaya ‘Davina’ wamejikuta wakitaka kuzichapa kavukavu baada ya
kushindwa kudhibiti hasira walipokuwa wakitaniana.
Irene
Paul Ishu hiyo ilitokea juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na mkusanyiko wa wasanii mbalimbali
ndipo wawili hao walipotunishiana misuli.
Halima
Yahaya ‘Davina’ Ishu hiyo iliibuka baada ya Davina kumtupia maneno ya
kejeli mwenzake huku Irene akionekana kuwa ‘siriaz’ akitahadharisha kuwa
hapendi utani na kuanza kumtupia maneno makali jambo lililowafanya
baadhi ya wasanii kutuliza hali ya hewa.
Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa.
Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa.

0 comments:
Post a Comment