Kundi
la muziki wa bongo flava nchini, Yamoto Band wanatarajia kukwea pipa
kwenda Afrika Kusini kwa ajili yakufanya video ya wimbo wao ‘Cheza kwa
Madoido’ na muongozaji mahili barani Afrika, Godfather.
Yamoto
Band ambao usiku wa kuamkia jana walitwaa tuzo ya Kili katika kipengele
cha ‘Kikundi bora cha muziki (Bongo Flava) wameamua kwenda Afrika Kusini
kufanya video ikiwa ni hatua za
awali za kuingia katika soko la
kimataifa.
Aidha Yamoto Band wameachia video ya wimbo wao mpya
unaoitwa ‘Nisambazie Raha’ unaofanya vizuri sana katika vituo vya radio
iliyofanyika chini ya uongozaji wake Isangi Mental.

0 comments:
Post a Comment