Monday, June 15, 2015

Tumejifunza nini vurugu za Port Said?

Zaidi ya hayo, mahakama hiyo iliwapeleka jela watu wengine 39 kwa vifungo vya muda tofauti huku wengine 20ishirini wakiachwa huru.

Wiki hii ulimwengu wa soka ulishuhudia uamuzi wa tofauti na mazoea, mahakama mjini Port Said huko Misri iliwahukumu kifo watu 11 ambao walitajwa kuhusika na vurugu zilizotokea uUwanjani huko Port Said mwaka 2012 kwenye mchezo wa soka baina ya wenyeji Al-Masry na National Al-Ahli.
Zaidi ya hayo, mahakama hiyo iliwapeleka jela watu wengine 39 kwa vifungo vya muda tofauti huku wengine 20ishirini wakiachwa huru.

Hukumu za masuala ya soka huishia na adhabu nyepesi zenye mwuelekeo huo kama vile mwashabiki na timu zao kutozwpigwa faini au timu kutakiwa kucheza mechi kadhaa bila mwashabiki na ammbo kuisha hivyo. Hukumu hii ya Mmahakama ya Port Said imeonyesha mwuelekeo tofauti kwambaambapo sasa hatua za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa hata kwa makosa ambayo yanaonekana kuwa yana sura ya kimchezo.

Hali ya kisiasa nchini Misri siyo tulivu, na inawezekana ikawa imeathiri mwenendo wa kesi na hukumu hiyo kali, lakini hakuna anayeweza kusema kama mahakama imetenda haki au imekandamiza upande wa mwashabiki. Hapa kwetu Tanzania, vurugu ni sehemu ya mchezo mzuri tunaoupenda na hata michezo mingine kama ngumi! Ningali mdogo, nilisikia sifa chafu za wachezaji na mwashabiki wa baadhi ya timu zaBoom na Ashanti za Ilala, na jinsi ambavo refa alikuwa akingelazimika kwenda kumaliza mpira getini katika Uwanja wa Karume ili kuanusuru nafsi yake dhidi yna waja wenye hasira.

Nimewahi kushuhudia mara moja jaribio la kumgawa mbuzi wa ushindi katikati kwa kuwa timu ya Texas Dume iliyopoteza mchezo haikuridhika na matokeo ya mechi yezo wa fainali.
Vurugu ni sehemu ya mchezo wetu na imekuwa ikisimuliwa kama pambo auma kinogesho cha mchezo wetu mbovu.

Ubaya wa masimulizi hiziaya ni kuwa yalisemwa kwa kusifia ukorofi, timu zenye washabiki wakorofi ndizo zilionekana za kijanja na zinazofaa kushabikia! Endapo hatua muhimu za kinidhamu hazitaanza kutekelezwa, ndani ya miaka kadhaa ijayo, tunaweza kushuhudia madhara makubwa sawa au kuzidi yale ya Port Said.

Haitashangaza mamlaka zetu zikaanza kukurupuka kutoa hukumu kwa watu na vilabu kama wenzao wa Misri, lakini tukumbuke kuwa Ligi Kuu nchini humo ililazimika kusimama kwa zaidi ya misimu miwili kutokana na fuatia dhahama ile ya Port Said.
Kwa miaka nenda rudi, mamlaka za soka zimekuwa zikiwavumilia mwashabiki wa Simba na Yanga ambao wamedai kuwa na majukwaa yao kwenye viwanja vya umma, wakianza na ule wa Uhuru na baadaye Uwanja wa Taifa.

Umiliki huu wa majukwaa hauishii kwenye maneno pekee, bali kwa vitendo kwani mtu asiye shabiki wa timu husika anapofika jukwaani hutolewa kwa ghasia na wakati fulani hata kuchaniwa jezi.
Utawala huu usio rasmi ni kwa mechi zote, hata ambazo zinahusisha Simba/Yanga dhidi ya klabu nyingine na zinazohusisha tTimu za Taifa.

Haki hii isiyo rasmi imewagharimu mwashabiki kadhaa utu wao kwa kusushwa, kuangushwa majukwaania, kuchaniwa jezi na kukosa amani na mchezo ambao wamelipa ili kuuona, tena kutoka kwa mwashabiki ambao hawajachangia senti moja kwenye ujenzi wa kiwanja.

Simba na Yanga hawajawahi kuwa na uwanja wenye hadhi kama wa Taifa, hivyo mwashabiki wake hawana uchungu na miundombinu hii kiasi kwamba hawaoni tabu kuvunja viti na kuharibu vyoo vya viwanja vya wenzao.

TFF na Bodi ya Ligi Kuu imekuwa ikiwakumbatia mwashabiki hawa na klabu zao, hata wanapowapa adhabu huwa siyo zenye lengo la kubadili hali ya usalama viwanjani.

Mamlaka hizi zimekataa Simba na Yanga kwenda kucheza mechi kwenye viwanja vya Manungu, Mabatini na Chamazi kwa kisingizio cha usalama kwa kuwa viwanja hivi ni vidogo. Kudai kuwa kigezo ni usalama mdogo ni kukiri kuwa wameshindwa kuwawekea utaratibu sahihi washabiki hawa, mbona mikoani kuna viwanja vidogo na Simba na Yanga wanacheza.

0 comments:

Post a Comment