BIASHARA
ya ngono imeshamiri mkoani Dodoma wakati huu ambao vikao vya kumpata
mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekwisha kuanza.Uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya kumbi kama Club ...., Club .... na ..... Lounge, Chako ...pamoja na Uhindini, umebaini kuwapo idadi kubwa ya kina dada wakiwa wamevaa nusu uchi.
Katika maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo hekaheka za wasichana wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja bila ya
wasiwasi wowote na wengine walisikika wakisema wako kibiashara na siyo kuuza sura.
Eneo maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha akina dada hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea magari huku wakitafuta wateja wenye magari.
Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema,‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?
‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume na wanatoa ‘mpunga’ nadhani huyu rais ajaye atakuwa na neema.’’
Dada mwingine ambaye aliyekuwa Dodoma... karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi, alisema ametoka Arusha akiwa na marafiki zake kwa lengo la kuwafuata wateja wa msimu walioko Dodoma.
Alisema hadi sasa ana siku tatu akiwa Dodoma na tayari amekusanya zaidi ya Sh 700,000 huku akiwatumia madalali ambao huwaunganisha kwa wateja
0 comments:
Post a Comment